Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amewasimamisha kazi Afisa Mifugo wa Wilaya ya Karatu, Mtendaji wa Kijiji pamoja na Afisa Mifugo wa kijiji, kutokana na uzembe wa kiutendaji, kwenye zoezi la kupiga chapa mifugo.
Gambo ametoa agizo hilo baada ya kugundua kuwa watendaji hao wa serikali walikuwa hawajatekeleza agizo la serikali la kupiga chapa mifugo, huku akiamuagiza Katibu Tawala wa Mkoa kumuandikia barua ya onyo Mkurugenzi wa Karatu.
“Nataka nikutaarifu kuwa kuanzia sasa namsimamisha kazi Afisa Mifugo wa wilaya, Mtendaji wa Kijiji hiki pamoja na Afisa mifugo anayehusika na kijiji hiki, lakini pia Katibu Tawala Mkoa amuandikie barua ya onyo Mkurugenzi wa Halmshauri ya Karatu, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashuri ya Karatu kwa hili,” amesema Gambo
Hata hivyo, Zoezi la kupiga chapa mifugo ni agizo kutoka serikalini ambapo mifugo yote nchini inatakiwa kupigwa chapa ili kuweza kutambua takwimu zake na kuepusha migogoro.