Kocha Mkuu wa Young Africans, Miguel Angel Gamondi, amesema ambacho anakihitaji kutoka kwa wachezaji wake wote wakiwemo Maxi Nzengeli na Yao Atttohoula kuhakikisha wanacheza mchezo unaovutia kwenye mechi zao zote.

Gamondi ambaye amerithi mikoba ya Nasreddine Nabi raia wa Tunisia ambaye alikiongoza kikosi hicho kwa misimu miwili na mafanikio yake makubwa ni kucheza Fainali Kombe la Shirikisho Barani Afrika 2022/23, Young Africans ikagotea ushindi wa pili.

Kocha huyo amesema wachezaji wa timu hiyo wanafanya kazi kubwa kwenye mechi zote, kitu ambacho ni muhimu kuwa endelevu.

“Kwenye kila mechi ambazo tunacheza wachezaji wanafanya kazi kubwa kusaka ushindi, hili ni muhimu kuwa katika hali endelevu kila wakati kwa kuwa matokeo yanapaswa kuwa mazuri.

“Mpira mzuri na unaovutia unahitajika kwetu, furaha yetu ni kuona tunatoa burudani kwa mashabiki na ushindi kupatikana kwenye mechi zetu za ushindani,” amesema Gamondi.

Jana Jumatano (Agosti 23), Young Africans ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, walianza kwa kishindo kutetea Ubingwa wa Ligi kuu Tanzania Bara kwa kuichapa KMC FC FC 5-0 kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar.

Azam FC kulipa kisasi Azam Complex
Wamiliki Vituo vya kulea watoto waonywa