Kocha Mkuu wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans Miguel Angel Gamondi, amesema hana haraka na Mshambuliaji wake, Mghana, Hafiz Konkoni kwani anaamini atampa anachotaka.

Gamondi amesema, anafahamu mchezaji huyo ni mzuri, ndiyo maana yupo kwenye klabu hiyo, ila kwa sasa anahitaji muda kidogo ili kuwa bora na kufunga mabao kama ambavyo anatakiwa kufanya.

“Sina shida na Konkoni, ni mchezaji mzuri ambaye kwa sasa anahitaji muda kutoa kitu ambacho watu wanahitaji. Najua mashabiki bado hawajapata kitu bora sana kutoka kwake.

“Ili aweze kufika huko, anahitaji muda, ndiyo maana nimekuwa nikimpa nafasi yeye pamoja na wenzake wote kwenye kikosi.” Amesema Kocha huyo kutoka nchini Argentina

Konkoni amecheza mechi mbili za ligi kuu na kufunga bao moja, lakini bado kumekuwa na mashaka kutoka kwa mashabiki ambao wamekuwa wakitarajia mabao mengi kutoka kwake.

Shaka amtembelea mtoto aliyechomwa moto
Utumishi wahimizwa ushirikiano kuongeza ufanisi wa kazi