Kocha Mkuu wa Young Africans, Miguel Gamondi, ameweka mitego yake kuelekea mchezo wa hatua ya kwanza wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika dhidi ya Al Merrikh akisema malengo yake ni kuona wanaendelea kucheza katika kiwango kizuri.
Young Africans wameanza vema msimu huu ambapo katika Ligi Kuu Bara, mpaka sasa wanaongoza wakiwa na alama sita, huku wakiiondosha ASAS katika hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Katika mechi nne ilizocheza za kimashindnao, Young Africans imefunga mabao 17 na kuruhusu moja.
Gamondi amesema: “Tunatamani kuona Young Africans ikiwa inacheza hivi katika mfululizo wake, tunatamani katika mashindano yale yakimataifa pia iwe kama katika ligi ambao huwa tunaamini ushindani hubadilika kulingana na mpinzani tutakayekutana naye.”
“Kikubwa ni kuzidi kutengeneza mipango na mbinu sahihi, wachezaji wapo tayari, nimeliona hilo, viongozi na sisi benchi la ufundi tupo tayari mashabiki wao wanatakiwa kusubiri kupokea ubora huu, tunashukuru kwa kuwa wamekuwa wakituunga mkono.”