Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans wameshamalizana kimazungumzo na Kiungo Mzawa, Jonas Mkude lakini imeliacha faili lake kwa Kocha Miguel Gamondi afanye uamuzi wa mwisho muda wowote juma hili atatangazwa.

Mkude aliitumikia Simba SC kwa zaidi ya miaka 10 kwa mafanikio, lakini klabu hiyo ya Msimbazi ilimtema ikiwa ni sehemu ya kujipanga upya baada ya kupoteza makombe kwa msimu miwili mfululizo.

Habari za uhakika kutoka ndani ya Young Africans zinadai baada ya majadiliano ya muda mrefu baina ya Mkude na klabu hiyo, na sasa inasubiriwa kauli ya Gamondi ili Mkude asaini na kutangazwa.

Uwezekano wa Mkude kusainishwa ni mkubwa kutokana na uzoefu wake ambao hata Gamondi ameelezwa lakini hata gharama yake ni ndogo kwani yuko huru na amekubaliana na masharti ya Young Africans.

Young Africansa itampa Mkataba wa mwaka mmoja wenye masharti ya kumuongeza kama kiwango kitamridhisha Kocha Miguel Gamondi.

Usajili wa Mkude unaenda kuongeza ushindani kwenye kiungo alipo Khalid Aucho na Yanick Bangala na mastaa wengine.

Real Madrid yang'ang'ana na Vinicius Junior
Miili 22 yapatikana awamu ya nne ufukuaji makaburi