Uongozi wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara umekiri kuumizwa na kitendo cha kupoteza Ngao ya Jamii ambayo walilishikilia kwa misimu miwili, lakini wamefurahishwa na kiwango kilichooneshwa na kikosi chao.
Makamu wa Rais wa klabu hiyo, Arafat Haji amesema licha ya kupoteza taji hilo, lakini wako timamu wakiwa na matumaini na soka la kocha mpya, Miguel Gamondi.
Arafat amesema wameyapokea matokeo hayo kwa kuwa ndio sehemu ya ushindani, lakini uongozi wao uko pamoja na wachezaji na benchi la ufundi chini ya Gamondi kutokana likosa kuamua mchezo pekee ndani ya dakika 90 hasa mechi hiyo, ila wanafahamu kwamba wamewaachia maswali mazito wapinzani wao kwa timu yao jinsi ilivyocheza mechi mbili.
“Tumeumia kupoteza hii Ngao, lakini kiukweli tuna matumaini makubwa na timu yetu. Tungefungwa ndani ya dakika 90 tungesema kuna shida mahali, lakini sote tunafahamu Penati hazina mwenyewe,” amesema Arafat.
“Timu yetu imecheza mpira mkubwa. Tunajua (Simba) wanashangilia kuchukua Ngao, lakini kwenye mioyo yao wanajua ni namna gani waliteseka kwenye mchezo ule. Viongozi wao tulikuwa nao pale juu (jukwaani Uwanja wa Mkwakwani) tuliwaona.
Neymar kujimwambafai Saudi Arabia
“Tunajivunia sana wachezaji na makocha wetu. Tunafahamu walimu wamejua wapi kuna shida ili wakati mwingine tuimalize mechi mapema na jambo zuri hili limetokea mapema tutarudi na nguvu kubwa kwenye ligi.”