Kocha Mkuu wa Young Africans, Miguel Gamondi amewataka wachezaji wake kupunguza makosa ambayo huwa yanafanyika kwenye mechi za Ligi Kuu na katika mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika uliochezwa nchini Algeria ljumaa iliyopita dhidi ya CR Belouizdad.
Amesema kuna wakati wachezaji wake wanakuwa hawana nidhamu ya mchezo na kutaka kufanya vitu vingi visivyohitajika uwanjani, kitu ambacho katika mechi za Ligi kuu huwezi kuadhibiwa kwa sababu ya baadhi ya viwango vya timu nyingi si bora, lakini vinakuja kuonekana na kuadhibiwa Ukikutana na timu kubwa na bora.
“Nidhamu kwenye mchezo ni kitu muhimu na hasa unapocheza na timu kubwa na bora hata Afrika, katika mechi iliyopita tumefungwa mabao 3-0 kilichotugharimu ni nidhamu ya mchezo, makosa machache tu Ukiyafanya kwa timu kama hizo wanakuadhibu.
“Unaweza usipate adhabu au kujua kama umefanya makosa kama ukicheza na timu za kawaida, hasa nyingi za Ligi Kuu na si wacheze kwa umakini, nidhamu kubwa na kutofanya makosa madogo madogo kama yale ya mechi iliyopita.
“Ninawapa mbinu ya kucheza kwa nidharnu ya mchezo, ni wakati gani wa kushambulia na wa kutulia, kumiki mpira au kupumzika, tukifanya hivi nadhani tutashinda mchezo wetu dhidi ya Al Ahly,” amesema.
Kocha huyo amesema amekuwa akifuatilia mechi za wapinzani wao kila wanapocheza na leo usiku ataifuatilia Al Ahly ikicheza mechi ya Ligi Kuu Misri dhidi ya Smouha.
“Nimewafuatilia wapinzani wetu, wako vizuri tunatakiwa kuwa makini kwa sababu ya ubora wao, tulifanya makosa mechi iliyopita kwa kutokuwa na nidhamu ya mchezo na kupoteza.