Kocha Mkuu wa Young Africans, Miguel Gamondi hana hofu kabisa ya kumkosa beki wake wa kati, Bakari Mwamnyeto katika mchezo dhidi ya AI Merrikh ya Sudan akitamba kuwa wapo mabeki wengine watatu watakaocheza nafasi yake vizuri.

Timu hizo zinatarajiwa kuvaana kesho Jumamosi (Septemba 16) majira ya saa 10 kamili jioni kwenye Uwanja wa Kigali Pele nchini Rwanda.

Young Africans na Al Merrikh ambao ndio wenyeji wa mchezo huo, zitavaana katika mchezo wa kuwania kufuzu Hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Gamondi amesema kuwa anajivunia wigo mpana wa kikosi chake kinachoundwa na wachezaji wengi wenye uzoefu na uwezo wa kucheza michuano ya kimataifa.

Gamondi amesema kuwa kabla ya kumruhusu Mwamnyeto, alichukua tahadhari mapema ya kuwaandaa mabeki wengine wa kati Dickson Job, Ibrahim Bacca na Gift Fredy kwa kuwatengenezea muunganiko mzuri wa kucheza kitimu.

Ameongeza kuwa hana hofu ya mabeki hao, kwani wamewahi kucheza pamoja katika baadhi ya michezo ya mashindano na kupata matokeo mazuri, hivyo mashabiki waondoe hofu.

Mwamnyeto amepata matatizo ya kifamnilia, isingekuwa rahisi kuwa na mchezaji katika msafara akiwa ana matatizo, hivyo nimeona nimpe ruhusa ya kwenda kumaliza matatizo hayo.

“Mashabiki waondoe hofu ya mchezo huo, kwani tayari ninao mabeki wengine wa kati wenye ubora na uzoefu wa kutupa matokeo mazuri katika mchezo huo ambao muhimu kwetu kupata ushindi.

“Uzuri katika kikosi changu nimetoa nafasi ya kila mchezaji kupambania namba, ili apate nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza, hivyo akikosekana mmoja anakuwepo mwingine ambaye ni bora zaidi,” amesema Gamondi.

Rupia kuongeza nguvu Singida Fountain Gate
Richarlison: Ninahitaji tiba ya kisaikolojia