Kocha Mkuu wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans, Miguel Gamondi amesema kikosi chake kipo tayari kwa Michuano ya Kimataifa sambamba na kuanza Ligi Kuu 2023/24.

Gamondi ametoa kauli hiyo akiwa jijini Tanga ambapo kikosi chake kilikuwa na mtihani wa kutetea Ngao ya Jamii, lakini kimeshindwa baada ya kufungwa na Simba SC kwa changamoto ya mikwaju wa Penati jana Jumapili (Agosti 13).

Kocha kutoka nchini Argentina amesema hana wasiwasi na ubora wa wachezaji wake ndani ya kikosi hicho na viongozi wake walimsajilia timu bora yenye vijana wenye njaa na mafanikio.

Ameongeza mechi ambazo wamecheza za kirafiki ukiongeza na zile za michuano ya Ngao ya Jamii zimewasaidia kuboresha ubora wa kikosi hicho na sasa wanawasubiri wapinzani wao KMC FC ambao ndio watafungua nao pazia la ligi.

“Tunajua sisi ndio watetezi, hivyo kila mmoja liglakinilataka kujua tunaanzaje kwetu tumemaliza maandalizi na sasa tupo tayari kwa mashindano.”

“Nina furaha na uwajibikaji wa wachezaji katika kipindi chote tulichokuwa kwenye mazoezi tuna wachezaji wanaojua wajibu wao kwa kuanza kushindana kwenye mazoezi, hili ni bora sana.” Amesema Gamondi

Upande wa Kimataifa Young Africans itacheza na Mabingwa wa soka nchini Djibout ASAS Sabieh mwishoni mwa juma hili.

Mashujaa FC watamba kukinukisha Ligi Kuu
Mandonga: Sijapata taarifa za TPBRC