Kocha Mkuu wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans Miguel Angel Gamondi amesema kikoisi chake kitalazimika kupambana na kupata ushindi katika mchezo wa Mzunguuko watatu wa Kundi D, Ligi ya Mabingwa Barani Afrika dhidi ya Medeama SC ya Ghana.

Young Africans itacheza mchezo huo Kesho Ijumaa (Desemba 08) katika mji wa Kumasi-Ghana, ikiwa inahitajika kupata ushindi ili kufufua matumaini ya kuwa moja ya timu mbili zitakazofuzu Hatua ya Robo Fainali, kutokea Kundi D.

Gamondi ameweka wazi mpango huo wa ushindi alipozungumza katika Mkutano  na Waandishi wa Habari mjini Kumasi akisema: Makundi  kuwa mgani “Ni lazima tushinde mechi yetu ya kesho mbele ya Medeama ili tufuzu hatua inayofuata, najua sio rahisi ila tutaweza kesho kupata alama, tumepata alama moja kwenye kundi ila timu yetu imefanya vizuri kwenye michezo iliyopita”

“Leo ndio nitajua kwenye maandalizi yetu ya mwisho nini nitaenda kufanya ila alama tatu za kesho ni lazima kwa sababu ni muhimu kwetu.”

“Tunajua kundi letu ni gumu maana lina CR Belouizdad na Al Ahly timu ambazo zina uzoefu mkubwa wa mashindano haya ya CAF Champions League, wana uwezo mkubwa wana kila kitu na uzoefu wao sio wa kulinganisha na sisi, ila niwaambie tu tunaanza hapa Medeama SC kusaka alama tatu pamoja na michezo yetu ijayo ya kundi hili na imani yangu inaniambia tutafuzu katikati yao CR Belouizdad na Al Ahly”

Basena ameacha ujumbe mzito Ihefu FC
TANAPA yaguswa tukio la mafuriko Hanang'