Mshambuliaji wa pembeni kutoka nchini Wales Gareth Frank Bale usiku wa kuamkia leo aliweka rekodi mpya katika maisha yake ya soka, baada ya kufunga bao la 200 tangu alipoanza kucheza soka mwaka 1999 akwa na klabu ya Southampton.

Bale alifunga bao hilo katika mchezo wa Europa League dhidi ya LASK ambao walilazimisha sare ya mabao matatu kwa matatu dhidi ya Tottenham Hotspur waliokuwa ugenini, jana Alhamis.

Bale mwenye umri wa miaka 31, kwa mara ya mwisho alifunga bao la 199 mwezi Novemba kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England, dhidi ya Brighton And Holve Albion, waliokubali kichapo cha mabao mawili kwa moja.

Mbali na kuandika rekodi katika masiaha yake kwa kufikisha mabo 200, mshambuliaji huyo pia amefaniiwa kufunga bao la ugenini kwa mara ya kwanza, baada ya kufanya hivyo alipofunga hat-trick kwenye uwanja wa San Siro nchini Italia mwaka 2010.

Bale anaitumikia Tottenham Hotspur kwa mkopo akitokea kwa mabingwa wa soka nchini Hispania Real Madrid, na kama ataonesha kiwango ktakachowavutia Spurs, huenda akabakia jumla klabuni hapo.

PICHA: Lwandamina atua Mwanza
IGP Sirro afanya mabadiliko jeshi la polisi

Comments

comments