Baada ya kuhusishwa na taarifa za kuwaniwa na mashetani wekundu (Man Utd) katika kipindi hiki cha usajili wa majira ya kiangaji, mshambuliaji wa pembeni kutoka nchini Wales na klabu ya Real Madrid Gareth Bale ametangaza msimamo wake, kwa kusema hafikirii kuondoka Santiago Bernabeu.
Bale ambaye alicheza mchezo wa kuwania European Super Cup usiku wa kuamkia hii leo dhidi ya Man Utd, amesema hataki kuondoka nchini Hispania kwa sasa kutokana na kuamini kwamba, bado ana uwezo wa kuitumikia Real Madrid ambayo inahitaji kutwaa mataji mengi zaidi.
Bale alimaliza utata huo baada ya kubanwa na waandisshi wa habari mara baada ya mchezo huo ulioshuhudia Man utd wakilazwa mabao mawili kwa moja kumalizika, ambapo jambo lingine amesema hakuwani kuzungumzana kiongozi yoyote kuhusu mpango wa kuondoka Real Madrid.
“Nitaendelea kuwa hapa, sina mpango wa kuondoka kwa sababu ninahitaji kutwaa mataji mengi zaidi nikiwa na Real Madrid ambayo pia inahitaji mchango wangu katika kipindi chote nitakachokuwepo Hispania.
“Sikuwahi kuzungumza na yoyote kuhusu suala la kutaka kuihama klabu hii, nilishangazwa sana kuona taarifa zangu katika vyombo vya habari zikiainisha mpango wa kutaka kuihama Real Madrid na kurejea England kwenye klabu ya Man Utd.
“Ninawahakikishia nipo Real Madrid na nitaendelea kuitumikia klabu hii.” Alisema Bale.
Bale alijiunga na Real Madrid mwaka 2013 akitokea Tottenham Hotspurs kwa ada ya pauni milioni 85.3 sawa na Euro milioni 100, ambayo kwa wakati huo ilimuweka mchezaji huyo katika rekodi ya dunia.