Mshambuliaji wa pembeni wa klabu ya Real Madrid, Gareth Bale ametajwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Wales ambacho kitakabiliwa michezo miwili ya kuwania kufuzu fainali za mataifa ya barani Ulaya za mwaka 2016, dhidi ya Bosnia-Herzegovina pamoja na Andorra.

Bale mwenye umri wa miaka 26, ametajwa kwenye kikosi cha timu ya taifa lake, huku akiwa hajacheza michezo mitatu iliyopita kwenye klabu ya Real Madrid kutokana na majeraha ya kiazi cha mguu ambayo aliyapata wakati wa mchezo wa mzunguuko wa kwanza wa ligi ya mabingwa barani Ulaya hatua ya makundi dhidi ya Shakhtar Donetsk.

Hata hivyo mshambuliaji huyo ameripotiwa kuwa tayari kucheza mwishoni mwa juma hili baada ya kupona jeraha la kiazi cha mguu na huenda akawa sehemu ya kikosi cha Real Madrid ambacho kitapambana na Atletico Madrid.

Mwingine aliyetajwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Wales baada ya kupona majeraha ni kiungo wa klabu ya Liverpool, Joe Allen pamoja na Joe Ledley wa klabu ya Crystal Palace.

Timu ya taifa ya Wales ambayo ipo chini ya kocha Chris Coleman, inahitaji point moja ili kukamilisha safari ya kuelekea nchini Ufaransa zitakapocheza fainali za mataifa ya barani Ulaya mwaka 2016.

Wales watawakabili Bosnia-Herzegovina siku ya jumamosi mjini Zenica na Oktrba 10 watakabiliana na Andorra kwenye jiji la Cardiff nchini Wales.

Kikosi kamili kilichotajwa tayari kwa michezo hiyo miwili upande wa makipa yupo Wayne Hennessey, Daniel Ward na Owain Fôn Williams.

Mabeki: Ashley Williams, Ben Davies, James Chester, James Collins, Chris Gunter, Neil Taylor, Ashley Richards na Adam Henley.

Viungo: Joe Allen, Aaron Ramsey, David Edwards, Andy King, Joe Ledley, Emyr Huws, Jonathan Williams na David Vaughan.

Washambuliaji: Hal Robson-Kanu, Simon Church, David Cotterill, Tom Lawrence, Sam Vokes na Gareth Bale.

Mashabiki Wakiri Kuchoshwa Na Brendan Rodgers
Mashabiki England Washangaa Sturridge Kuachwa