Hatimaye Nahodha na Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Wales Gareth Bale ametangaza kustaafu soka akiwa na umri wa miaka 33, baada ya kufanya kazi kubwa akiwa na timu hiyo.

Bale ametangaza maamuzi hayo, huku akiacha kumbukumbu ya kuwa Mchezaji wa kiume aliyecheza michezo mingi zaidi akiwa na Timu ya Taifa ya Wales, huku akifunga mabao 44 katika michezo 111 aliyoicheza timu hiyo.

Mshambuliaji huyo ametangaza maamuzi ya kujiweka Pembeni kuutumikia mchezo wa Soka, kupitia kurasa zake za Mitandao ya Kijamii, ambako aliamini ndiko Mashabiki wake wengi wangeona mapema uamuazi wake.

“Baada ya kutafakari kwa kina, natangaza rasmi kustaafu Soka, kwa sababu ninaamini ni muda sahihi kwangu kufanya hivi,”

“Ninajisikia mwenye bahati sana kutimiza ndoto yangu ya kucheza mchezo ninaoupenda ‘Soka’.” ameandika Bale aliyetwaa Taji la ubingwa mara tano wa Ligi ya Mabingwa akiwa na Real Madrid

“Kwa kweli [mpira wa miguu] umenipa baadhi ya nyakati bora zaidi za maisha yangu,”
“Kiwango cha juu zaidi cha misimu 17, haitawezekana kuiga, haijalishi ukurasa unaofuata umeniandalia nini.” aliongeza Bale.

Maisha ya Soka ya Bale mzaliwa wa Cardiff yalianzia katika Klabu ya Southampton (2006–2007) na baadae alihamia Tottenham Hotspur jijini London (2007–2013).

Mwaka 2013 aliweka Rekodi ya kuwa Mchezaji aliyesajiliwa kwa fedha kubwa akihamia Real Madrid kwa ada ya Pauni Milioni Milioni 80.

Hadi anatangaza kustaafu Soka Bale alikuwa anaitumikia Klabu ya Los Angeles FC ya Marekani.
Msimu wa 2020–2021 Real Madrid ilimrudisha kwa mkopo Tottenham Hotspur, ambapo kwa kipindi hicho alicheza michezo 20 na kufunga mabao 11.

Upande wa Timu ya Taifa ya Wales Bale ameichezea timu hiyo kwenye Fainali za Barani Ulaya ‘ Euro’ za mwaka 2016 na 2020 kabla ya kushiriki kwa mara ya kwanza katika Fainali za Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar.

Hata hivyo Wales iliwahi kushiriki Fainali za Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza kama nchi mwaka 1958.
Bale alitangazwa kuwa mwanasoka bora wa mwaka mara mbili akiwa Tottenham, 2010-11 na 2012-13.

Akiwa Real Madrid, Bale alikuwa sehemu ya kikosi cha Klabu hiyo kilichotwaa Ubingwa wa La Liga mara matatu.

Chelsea yavuruga dili la Joao Felix
Ally Kamwe afichua usajili Young Africans