Mshambuliaji wa pembeni wa Real Madrid  Gareth Bale amewaomba radhi viongozi, mashabiki na wachezaji wa klabu hiyo, kufuatia kuonyeshwa kadi nyekundu wakati wa mchezo wa ligi ya nchini Hispania, uliochezwa usiku wa kuamkia leo dhidi ya Las Palmas.

Mchezo huo ulimalizika kwa Real Madrid kulazimisha sare ya mabao matatu kwa matatu na kutoa mwanya kwa mahasimu wao FC Barcelona kuongoza msimamo wa ligi, kutokana na ushindi mabao sita kwa moja walioupata dhidi ya Sporting Gijon.

“Siamini kama kosa nililolifanya limenisababishia kadi nyekundu. Nilipaswa kuadhibiwa kwa kadi ya njano, kwa sababu nilisukumwa na mimi nikamsukuma mpinzani wangu. Natambua nimefanya makosa makubwa sana kwa adhabu hii, sina budi kumtaka radhi kila mmoja ambaye aliumizwa na kitendo cha kutoka kwangu, na pengine huenda ilikua chanzo cha kupata matokeo ambayo hatukuyatarajia.”

“Tuna mchezo mgumu mwishoni mwa juma hili, tutacheza dhidi ya Éibar na siku mbili baadae tutapambana na SSC Napoli katika michuano ya ligi ya mabingwa. Tunapaswa kupambana vilivyo ili tupate ushindi na kuendelea kuwa sehemu ya kuwania ubingwa wa La Liga msimu huu.” Alisema Bale

Kwa upande wa mlinda mlango wa Real Madrid Keylor Navas alisema: ” Bale amejaribu kuzungumza na kila mtu tulipokua katika vyumba vya kubadilishia, na ametutaka msamaha kwa makosa aliyoyafanya. Tumeungana kwa pamoja na kumwambia hapaswi kufanya jambo hilo kwa sababu kila mmoja anatambua kufanya makosa ni sehemu ya mchezo.

Oprah Winfrey auwaza Urais wa Marekani, Trump achangia
Arsene Wenger: Sina Mpango Wa Kuondoka Arsenal