Baada ya kulala kwa kichapo cha goli 2-1 dhidi ya Iceland na Roy Hodgson kujiuzulu nafasi ya ukocha, Chama cha soka nchini England kinajiandaa kumtangaza Gareth Southgate kuwa kocha wa muda wa timu yake ya taifa katika mwanzo wa kampeni za kuwania kufuzu kombe la dunia.

Zoezi la kumsaka kocha mpya litaanza baada ya michezo ya awali ya kufuzu kufanyika.

Mtendaji mkuu wa FA Martin Glenn,amesema kuwa kupatikana kwa kocha mpya kunaweza kuchukua miezi kadhaa,huku pia akimtaja meneja wa Arsenal, Arsene Wenger ambaye anaingia katika mwaka wa mwisho wa mkataba wake kama moja ya chaguo lao.

Roy Hodgson alijiuzulu baada ya kukifundisha kikosi cha England kwa miaka mitatu kufuatia kichapo dhidi ya timu ndogo ya Iceland mjini Nice siku ya Jumatatu.

 

Video: Serikali kuwatengea maeneo zaidi wachimbaji wagodo wa Madini nchi nzima
Fastjet yatangaza punguzo kubwa la nauli mwezi Septemba kwa ‘maelfu ya siti’, Wahi dili