Serikali Nchini, imeutaka Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa, kuacha kulitumia Magari ya Wagonjwa kwa shughuli nyingine, ikiwemo kubeba Watumishi, wakati wa utekelezaji wa majukumu mbalimbali.

Wito huo, umetolewa na wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Rudi katika ziara yake ya kikazi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Shule ya Msingi ya Chilendu, iliyopo Jimbo la Kibakwe – Mpwapwa.

Amesema, ni jambo la aibu kuona Gari la kubebea wagonjwa likitumika kwa ajili ya kufanyia mambo mengine, huku kusudio la msingi likiwa limeachwa la kubeba Wagonjwa kitu kinachohatarisha maisha ya akina Aama Wajawazito na wagonjwa wengine mahututi.

Hata hivyo, Simbachawene ambaye alishangaa kuona Gari moja la wagonjwa la kituo cha Afya cha Rudi na kuwataka Viongozi hao kulitumia kwa lengo lililokusudiwa, ili kusaidia kupunguza vifo vya Wajawazito na Wagonjwa wengine pindi linapohitajika kwa dharula na kawaida.

Waziri apokea taarifa hali ya upatikanaji wa Umeme
Mradi wa Bil. 42 kusaidia uvutaji Maji Ziwa Victoria