Watu watatu watumishi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) wamefariki dunia baada ya gari walilokuwa wakitumia kwenye doria kuacha njia na kutumbukia baharini
Imeelezwa kuwa ajali hiyo imetokea kwenye gati namba zero katika bandari ya Dar es Salaam, Eneo ambalo lina kina cha maji mita 14.
Ajali hiyo imetokea juzi, Aprili 18, 2020 majira ya saa tatu usiku, miili ya marehemu imehifadhiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili.