Mchezaji wa zamani wa Manchester United, Gary Neville, anaamini kwamba ni ngumu kwa klabu hiyo kumaliza katika nafasi tano za juu msimu huu baada ya mwanzo mbaya kwenye Premier League.
Akizungumza kwenye Podcast yake iliyoandaliwa na Kituo cha Sky Sports, Gary Neville alisema kuwa: “Sidhani kama Manchester United itamaliza katika nafasi tano za juu msimu huu. Nadhani wako mbali sana.
“Na ninashangaa kwa sababu wiki kadhaa zilizopita nilikuwa nawaweka katika nafasi tatu za juu, lakini kiukwei kwa ninachokiona kwa sasa, sidhani kama kipa yuku sawa.
“Ikiwa kipa wako hayuko sawa na timu haina utulivu, husababisha shida kubwa. Imewahi kunitokea wakati naitumikia United. Kwa hivyo United, kwangu mimi haiko sawa,” alisema Neville.
United waliibuka na ushindi kwenye mechi yao ya mwisho ya Ligi Kuu England dhidi ya Brentford, kupitia bao la dakika za lala salama kutoka kwa Scott McTominay.
Presha kubwa imetanda juu ya usalama wa Erik ten Hag katika msimu wake wa pili akiwa United na ikiwa kocha huyo atashindwa kufuzu kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, huenda kibarua chake kikaota mbawa.