Gwiji wa Klabu ya Manchester United, Gary Neville amesema kipa Aaron Ramsdale ambaye aliiweka Arsenal kwenye nyakati nzuri kutokana na uchezaji wake kwenye sare ya 2-2 dhidi ya Liverpool Jumapili (April 09), anaweza kuwa sababu ya Arsenal kuwa bingwa msimu huu.

Neville amempongeza Ramsdale kwa uokoaji wake mzuri katika dakika za mwisho za mechi yao wakiwa Anfield na kuwapa alama moja Arsenal akiongeza kuwa kwa ushujaa wa kipa huyo wababe hao wa London wanaweza kuwa mabingwa.

“Nadhani leo (juzi) ni hatua nzuri kwao,” alisema na kuongeza: “Mambo hutokea katika uwanja huu (Anfield) ambayo hayafanyiki katika uwanja mwingine wowote.

“Arsenal wamefanya kazi ila Ramsdale namna ambavyo amecheza anaweza kuwapa ubingwa Arsenal.”

Panga pangua ya Erik Ten Hag 2023/24
Inatisha: Idadi ya vifo Ukraine yakaribia watu 8,500