Gavana wa Benki Kuu Tanzania, Profesa Florens Luoga ameipongeza Mamlaka ya Kudhibiti Ununuzi wa Umma (PPRA), kwa kazi wanayoifanya ya kusimamia sheria ya ununuzi wa umma.

Akizungumza leo, Agosti 7, 2020 alipotembelea banda la Mamlaka kwenye Maonesho ya 27 ya Wakulima, maarufu kama Nanenane, yanayofanyika kitaifa Mkoani Simiyu, Profesa Luoga alisema kuwa wanatambua kazi inayofanywa na PPRA katika kuhakikisha kuna thamani halisi  ya fedha kwenye ununuzi wa umma.

“Kweli kazi yenu tunaiona, mnafanya kazi nzuri. Zamani kidogo kulikuwa na changamoto, lakini kwa sasa kazi yenu tunaiona na tunaitambua, kwa hilo ‘we commend you’ (tunawapongeza),” amesema Profesa Luoga.

Akiwa katika banda hilo la Mamlaka, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sheria na Mahusiano kwa Umma, Bi. Winifrida Samba alimuelezea kuhusu huduma zinazotolewa na Mamlaka.

Pamoja na mambo mengine, Bi. Samba alimueleza Gavana wa Benki Kuu kuhusu ufanisi unaopatikana kwa kufanya ununuzi kupitia Mfumo wa Ununuzi kwa njia ya Mtandao (TANePS), ambapo Gavana huyo wa Benki Kuu alipongeza hatua hiyo kwani hivi sasa michakato ya ununuzi ianafanyika kupitia mfumo huo.

PPRA imehudhuria Maonesho ya Nanenane Kitaifa mkoani Simiyu ambapo imetoa elimu kwa umma kuhusu huduma zake na majukumu yake.

Aidha, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Uwekezaji Mhe. Angellah Kairuki pia alitembelea banda hilo, ambapo aliitaka PPRA kuendelea kuzisimamia taasisi nunuzi kuhakikisha zinatenga 30% ya ununuzi wake  wa mwaka mzima kwa makundi maalum, kama sheria inavyoelekeza. Makundi maalum hayo ni wanawake, wazee, vijana na watu wenye ulemavu.

“Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya Mwaka 2015 na sheria pia inazitaka taasisi nunuzi kutenga 30% kwa ajili ya makundi maalum, PPRA mnapaswa kuhakikisha mna ‘mechanism’ ya kufuatilia utekelezaji wake. Tuliwaahidi wananchi, tusimamie utekelezaji wake,” amesema Waziri Kairuki. 

Viongozi wengine waliotembelea banda la PPRA ni pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka, Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima, Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Dkt. Joseph Chilongani, Aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagin, Katibu Tawala wa Wilaya ya Busega, R. Rutagumirwa, Katibu Tawala wa Meatu, A. Rutaihwa.

Wadau na wananchi mbalimbali walipewa elimu na kuhamasishwa kuwa sehemu ya usimamizi wa ununuzi wa umma, kwa kutoa taarifa PPRA pale ambapo wataona kuna dalili za uvunjifu wa sheria.

Gavana wa Benki Kuu, Profesa Florens Luoga akisaini kitabu katiba banda la PPRA

Afisa Mifumo ya Tehama, Giftnes David alieleza kwa ufupi kuhusu ufanisi kuhusu ufanisi wa Mfumo wa Ununuzi kwa njia ya Mtandao (TANePS), ambapo Gavana huyo wa Benki Kuu alipongeza hatua hiyo.

PPRA imehudhuria Maonesho ya Nanenane Kitaifa mkoani Simiyu ambapo imetoa elimu kwa umma kuhusu huduma zake na majukumu yake.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Agosti 8, 2020
DC Joketi atoa fursa kwa vijana 150