Serikali imetangaza kulifungia gazeti la kila wiki la ‘Mawio’ linalomilikiwa na kampuni ya Victoria Media Services Limited, chini ya Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea.

Taarifa ya kufungiwa kwa gazeti hilo imetolewa na Wizara ya Habari, Utamaduni, Michezo na wasanii kupitia barua yake rasmi iliyosainiwa na waziri wa wizara hiyo, Nape Nnauye.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, gazeti hilo limepewa kifungo cha kudumu (permanent) kilichoanza rasmi Januari 15 mwaka huu.

Mawio Lafungiwa

Gazeti hilo limefungiwa kuchapishwa kwa njia yoyote ikiwa ni pamoja na kusambazwa kwa njia ya kielekroniki na njia ya posta.

Hivi karibuni, gazeti la Mwanahalisi ambalo ni gazeti dada la Mawio liliandika kuhusu dalili za kufungiwa kwa gazeti hilo na kueleza kuwa tayari serikali ilikuwa imemuandikia barua mhariri wa Mawio na kuwataka kujieleza kwanini huandika makala za kichochezi.

Kwa mujibu wa gazeti hilo, barua ya kujieleza ya mhariri wa Mawio ilijibiwa kuwa maelezo yake hayakuridhishwa.

Moja kati ya habari zilozotajwa kuwa ingeweza kuzua taharuki kwa wananchi, ni ile iliyoandikwa na gazeti la Mawio kuwa ‘Maalim Seif atatangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi wa Zanzibar.

Celine Dion aondokewa na kaka yake, siku mbili baada ya kumpoteza mumewe
Uhalifu: Wananchi wampiga Polisi na Kumpora bunduki

Comments

comments