Gazeti la Oftenspoten la nchini Norway ambalo ni la pili kwa umarufu nchini humo, limelazimika kutoa ufafanuzi na kuomba radhi baada ya kuchapisha taarifa za kifo cha ‘Father Christmas’.

Katika chapisho hilo, gazeti hilo lilieza kuwa kifo hicho ni cha Father Christmas ambaye alizaliwa Disemba 12 mwaka 1788 na kwamba alifariki Disemba 3 mwaka huu.

Walieleza kuwa ibada ya mazishi yake ilipaswa kufanyika Disemba 28 mwaka huu katika kanisa linalojulikana kama ‘North Pole Chapel’.

Gazeti hilo lililazimika kuomba radhi na kueleza kuwa kosa lililofanyika lilitokana na taratibu za utendaji kazi.

Taarifa rasmi ya gazeti hilo ilieleza, “Aftenposten ina taratibu kali kuhusu habari na kutumiwa kwa ishara na mifano katika matangazo yetu ya vifo. Tangazo hili linakiuka taratibu hizi na halikufaa kuchapishwa.”

Chanzo: BBC

 

 

Serikali Yawataka Wafanyakazi ‘Kuwasema’ Wakuu Wa Mikoa Wanaowaburuza Na Kuwatupa Selo
Picha: Kanye West Na Kim Kardashian Wapata Mtoto Wa Pili, Waonesha Picha