Timu ya Geita Gold FC leo Jumanne (Oktoba 04) imevuna ushindi wake wa kwanza, baada ya kuanza vibaya msimu huu 2022/23, kwa kuambulia matokeo ya vichapo na sare.

Geita Gold FC ikicheza nyumbani Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza dhidi ya Maafande wa Jeshi la Polisi ‘Polisi Tanzania’ imeibuka na ushindi wa 2-1.

Mabao ya Geita Gold yamefungwa na Mfungaji bora msimu uliopita George Mpole, dakika ya 45 na baadae Edmund John alifunga bao la ushindi, dakika ya 83.

Bao la kufutia machozi la Polisi Tanzania limefungwa na Hassan Kapona dakika ya 64.

Kwa matokeo hayo Geita Gold imefikisha alama sita zinazoiweka nafasi ya 13 kwenye msimamo, baada ya kushuka dimbani mara sita, ambapo imeshuhudiwa ikishinda mchezo mmoja, kupoteza miwili na kuambulia sare michezo mitatu.

Polisi Tanzania wamebaki nafasi ya 14 kwenye msimamo wa Ligi Kuu, wakicheza michezo mitano, wakipoteza mitatu na kutoka sare miwili.

Ally Kamwe aichimba mkwara Simba SC
Simba SC kwenda Angola kwa ndege maalum