Mchambuzi wa Michezo nchini Tanzania Geoffrey Lea ameingia wasiwasi dhidi ya Kikosi cha Young Africans kuelekea mchezo wa Mkondo wa Pili wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika dhidi ya Al Hilal ya Sudan.
Miamba hiyo ya Afrika Mashariki na Kati itakutana Uso kwa Macho Jumapili (Oktoba 16) katika Uwanja wa Al Hilal mjini Khatoum-Sudan saa mbili usiku kwa saa za Tanzania.
Geoffrey Lea ameonyesha wasiwasi huo baada ya Al Hilal kucheza mchezo wao wa kwanza wa Ligi Kuu nchini Sudan jana Jumatano (Oktoba 12) dhidi ya Wad Nobawi iliyokubali kichapo cha 4-0.
“Al Hilal wamecheza jana mechi ya ligi, Ndg zetu Watanzania wenzetu hawajacheza mechi yoyote tangu walipocheza mechi ya mwisho ya kiushindani, kiufundi hii haitawasaidia watanzania wenzetu maana wataingia wanakosa match fitness,anyway kila la kheri #AnythingIsPossible” ameandika Geoffrey Lea
Al Hilal itaikabili Young Africans huku ikiwa na faida ya matokeo ya sare ya 1-1, yaliopatikana ugenini Dar es salaam Jumamosi (Oktoba 08) kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa.