Beki wa FC Barcelona Gerard Pique amekubali kuna tatizo ndani ya kikosi cha klabu hiyo kwa sasa, hali ambayo imepelekea kupoteza mchezo wa Ligi ya Hispania dhidi ya Atletico Madrid mwishoni mwa juma lililopita.

Pique ambaye alikuazwa na klabu hiyo kupitia kituo cha ‘La Masia’ amesema mchezo dhidi ya Atletico Madrid umemthibitishia kuna tatizo kubwa ndani ya kikosi chao, na kuna haja likafanyiwa kazi mapema.

Amesema katika mchezo huo walicheza vizuri dakika za awali, lakini muda ulivyokua unakwenda, mambo yaliwaribikia na kutoa nafasi kwa wenyeji wao,kupata mabao mawili yaliyowapa ushindi.

“Tulianza vizuri, lakini walifunga mabao mawili yanayofanana,” alisema akiiambia Movistar.

“Mambo ni magumu sana kwa upande wetu. Tupo kwenye wakati mgumu na kuna matatizo kadhaa.”

“Watu tayari wanajua matatizo yetu. Hata mtu kipofu anaweza kuona nini tunachokikosa. Lakini tutarudi kwenye ubora wetu hivi karibuni.”

Barca walipiga mashuti mawili tu ya kulenga bao katika dakika zote 90 kwenye mchezo huo, uliopigwa Uwanja wa Wanda Metropolitano.

Memphis Depay, ambaye amekuwa na mashuti mengi ya kulenga bao kwenye LaLiga (13, sawa na Karim Benzema wa Real Madrdi, hakufurukuta kabisa kwenye mchezo huo.

Atletico walikuwa kwenye kiwango bora, wakifunga mabao mawili katika mashuti sita yaliyolenga bao, Luis Suarez alitengeneza bao la kwanza lililofungwa na Thomas Lemar kabla yeye kufunga la pili.

Barca sasa imeruhusu mabao matano bila wao kufunga katika mechi mbili zilizopita, na Pique, ambaye alikuwa sehemu ya kikosi wakati wakifungwa na Benfica kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya katikati ya wiki, amesema kikosi chao kinahitaji kufanya kazi ya ziada.

Kim Poulsen: Tutakusanya alama 9 nyumbani
Carlo Ancelotti akasirishwa Real Madrid