Baada ya Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dkt. John Mgufuli kuwasamehe wafungawa 5,533, jana katika maadhimisho ya miaka 58 ya uhuru wa Tanganyika, Gereza la butimba limetekeleza agizo hilo.

wafungwa 79 kati ya hao waliokuwa wamefungwa katika gereza la Butimba lililopo mkoani Mwanza wameachiwa mapema leo Desemba  10, 2019.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella amefika katika gereza la Butimba kwaajili ya kushuhudia utekelezaji wa agizo la Rais Magufuli huku mkuu wa gereza hilo, Hamza Hamza akibainisha idadi ya wafungwa waliochiwa kuwa ni 79.

Pia ametaja aina ya wafungwa waliopata msamaha wa Rais katika gereza hilo kama ambavyo Rais alielekeza na kuwakabidhi orodha yao.

“Wafungwa wengine ni wahamiaji haramu ambao wataachiwa huru lakini kwa kufuata taratibu za idara ya uhamiaji” amesema Hamza.

Rais Dkt. Magufuli alitangaza msamaha wa wafungwa katika maadhimisho hayo, akibainisha kuwa idadi hiyo ni kubwa kuwahi kutokea kuliko wakati mwingine wowote.

Kiongozi aliyepita bila kupingwa mbaroni kwa tuhuma za Wizi
Mamia waaga kwa majonzi Mwili wa Mufuruki

Comments

comments