Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi na Kifua Kikuu imeupongeza Mgodi wa Geita Geita Gold Mine kwa kutoa elimu ya Masuala ya Ukimwi na Kifua Kikuu kazini.

Pongezi hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Fatma Hassan Toufiq mara baada ya kupokea taarifa ya Utekelezaji wa Afua za Ukimwi na Kifua Kikuu katika moa wa Geita zinazofanywa na mgodi huo.

Toufiq amesema sehemu za Migodini huwa na watu wengi wanaopata maambukizi ya Kifua Kikuu kutokana na mazingira wanayofanyia kazi kuwana vumbi jingi na kuitaka Migodi kuboresha mazingira ya kazi kwa wafanyakazi ili kujiepusha na Ugonjwa wa Kifua Kikuu.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel ameitaka Migodi kutotiririsha maji taka yenye kemikali katika vyanzo vya maji ili kuwaepusha wananchi kupata maambukizi ya magonjwa mbalimbali ikiwemo Ugonjwa wa Saratani.

“Mikoa ya Kanda ya Ziwa inaonekana kuongoza kwa ugonjwa wa Saratani, tumeamua kufanya utafiti kujua nini kinasababisha tatizo hilo kukua kwa kasi kubwa maana ukija Hospitali ya Magonjwa ya Saratani ya Ocean Road wagonjwa wengi ni wa Kanda ya Ziwa” amesema Dkt. Mollel.

Kamati hiyo ilitembelea mgodi huo wa GGM, ili kuangalia miradi ya maendeleo inayofanywa na mgodi huo kwa wananchi wa mkoa wa Geita.

Biden:"Putin alikosea"
Mtoto wa Museven aunga mkono Uvamizi wa Urusi kwa Ukraine