Mlinda mlango mkongwe wa klabu ya Juventus, Gianluigi Buffon ametangaza kuondoka katika klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu baada ya kuitumikia kwa miaka 17.
Mpaka sasa Buffon amecheza jumla ya michezo 655 katika ngazi ya vilabu akiwa ameshinda vikombe 19. Mchezo wa Juventus dhidi ya Verona utakaopigwa Jumamosi hii utakuwa ndio mchezo wake wa mwisho akiwa kchezaji wa klabu hiyo.
Hata hivyo Buffon hajatangaza kutundika daruga pamoja na kuwa na umri wa miaka 40 kwani kuna vilabu ambavyo tayari vimeonyesha nia ya kuhitaji huduma yake.
? @gianluigibuffon: “Saturday will be my final match for Juventus and to end this journey with two cups and with the president and the entire Bianconeri world by my side, will be very special.”
— JuventusFC (@juventusfcen) May 17, 2018
Katika miaka yote 23 ambayo kipa huyo amekuwa dimbani, ni klabu mbili tu mabazo amezitumikia akianzia katika klabu ya Parma kabla ya Juventus kumsajili mwaka 2001 kwa kiasi cha paundi milioni 32.6 akiwa golikipa ghali zaidi, rekodi ambayo anaishikilia mpaka leo.
Buffon ni kati ya walinda mlango wenye rekodi za kipekee kabisa ambapo katika msimu wa ligi ya Serie A mwaka 2015/2016 aliweka rekodi ya kucheza dakika 974 bila kuruhusu goli.