Waziri Mkuu wa Italia Giuseppe Conte ametangaza rasmi kuwa timu zote za michezo zinaweza kuanza mazoezi tarehe 18 Mei mwaka huu, baada ya kutii agizo la serikali la kusimamisha shughuli za michezo, kwa lengo la kupisha vita dhidi ya maambukizi dhidi ya virusi vya Corona.
Ligi kuu ya Italia SerieA ilikua miongoni mwa shughuli za michezo zilizosimamishwa nchini Italia tangu Machi 9.
Serie A imebakiza mizunguuko kumi na mbili (12) kukamilisha msimu wa 2019/20, pamoja na michezo mingine minne ambayo iliahirishwa katika raundi ya 25. Kombe la Italia pia lilisitishwa baada ya mchezo wa kwanza wa nusu fainali.
Hatua hiyo inamaanisha kuwa michezo ya Serie A inaweza kuanza rasmi mwezi Juni, ingawa Waziri Mkuu wa Italia Giuseppe Conte amesema uamuzi juu ya kuanza kwa ligi hautafanywa hadi tarehe ya baadaye.
Conte amesisitiza kuwa serikali “itafanya kazi na wataalam” kuangalia hali hiyo na baadaye “kutathmini njia sahihi ya kumaliza msimu uliosimamishwa”.
Conte pia amesema kuwa wanamichezo watakuwa huru kuanza mazoezi binafsi kuanzia Mei 4 na Hiyo ndio tarehe rasmi ambayo raia nchini Italia wataweza kuruhusu.