Mbunge wa Arusha Mjini kupitia tiketi ya (CHADEMA), Godbless Lema amesema kuwa kitendo cha David Kafulila kuhama Chama hicho anaamini kuwa atamshauri mke wake naye afuate nyayo zake.

Kwenye ukurasa wake wa twiter, Lema ameandika ujumbe akisema Kafulila ni rafiki yake wa karibu, lakini kwa namna alivyoamua hana shaka atamshauri mke wake ambaye ni mbunge kupitia chama cha Chama hicho kufanya kama yale aliyoyafanya.

“Kafulila ni rafiki yangu, nafikiri kwa namna hii alivyoamua ataweza bila shaka kumshauri Mbunge wa Chadema, Jesca Kishoa (mke wake) kufikiri kama yeye, hii inaweza kusaidia maoni yake juu ya uamuzi aliouchukua na kuthibitisha ukweli huu kama hupo,”ameandika Lema

Hata hivyo, Kafulila alitangaza kukihama chama cha hicho akidai vyama vya upinzani havina nia ya kupambana na ufisadi, lakini mke wake Jesca Kishoa ambaye ni mbunge wa viti maalum kupitia Chama hicho bado hajazungumza chochote.

 

Kozi ya Grassroots yapelekwa Mbeya
Serikali yazuia utoaji fedha za wakandarasi