Wakati Ligi Kuu Tanzania Bara msim huu 2020/21 ikiesaliwa za mizunguuko minne kabla haijamalizika, huku ukuta wa Simba SC ukionekana ndio imara zaidi kwa kuruhusu idadi ndogo ya mabao hadi sasa, lakini kama unadhani hilo limefanya Kocha Didier Gomes abweteke basi pole yako, kwani Mfaransa huyo sasa ni kama anataka sifa!

Inaelezwa kuwa, kocha huyo amewaangalia mabeki wake wa kati waliopo kwa sasa kikosini, akiwamo Pascal Wawa, Joash Onyango, Erasto Nyoni, Kennedy Juma na Ame Ibrahim, lakini anawaambia mabosi wake, bado anataka kitasa kingine kipya chenye makali zaidi ya mabeki alionao.

Kutoka ndani ya Simba SC taarifa zinaeleza kuwa mabingwa hao wa Tanzania Bara mara tatu mfululizo, wanatafuta beki wa kati mwenye uwezo zaidi ya Wawa, katika kuokoa mipira ya chini na juu, kuanzisha mashambulizi, utulivu anapokuwa na mpira pamoja na kasi ya kuwazuia washambuliaji wasumbufu kama Jean-Marc Makusu anayetajwa kutakiwa na Young Africans.

“Kocha ametuambia kama tutakosa beki wa namna hiyo wala tusifikirie jambo lolote la mabadiliko katika eneo hilo, lakini kama tutampata tumpelekee jina lake na atamuangalia kama ataridhika naye hapo ndio atatoa uamuzi wa huyo mpya au atabaki na ambao tunao wakati huu,” kimesema chanzo hicho.

Simba SC inaendelea kuongoza msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa na alama 67, ikiaacha Young Africans kwenye nafasi ya pili ikiw ana alama 61 na Azam FC inashika nafasi ya tatu kwa kumiliki alama 60.

Hiki hapa kinachompeleka Mkude hospitali
Simba SC: Onyango hauzwi