Kocha mkuu wa Simba SC Didier Gomez Da Rossa amekiri haikuwa rahisi kufanikisha ushindi dhidi ya Dodoma Jiji FC ambao walikua nyumbani Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma jana jioni.

Gomez ambaye alikua na kibarua cha kwanza cha Ligi Kuu tangu alipowasili nchini mwezi uliopita, amesema alijipanga vilivyo kuelekea mchezo huo ambao alitambua ungekua mgumu katika muda wote wa dakika 90.

Amesema wachezaji wake walifuata maelekezo yote aliowapa kabla ya mchezo huo kuanza na  wakati wa mapumziko, hivyo hana dundi kuwapongeza kwa kazi kubwa ambayo imepawa alama tatu muhimu ugenini.

“Tulitambua kwamba utakuwa mchezo mgumu tangu awali kwa kuwa ligi ipo tofauti na ni ngumu, kila timu inahitaji pointi tatu hivyo nimeona wachezaji wangu walipambana.”

“Kwa ushindi wa mwanzo sasa hapo tunageuza nguvu zetu kwenye mchezo wetu ujao dhidi ya Azam FC kwani lengo la kwanza ni pointi tatu kisha mambo mengine yanafuata.”

“Hii itatusaidia kupunguza pointi ambazo tumeachwa na yule anayeongoza ligi hivyo bado tuna kazi kubwa ya kufanya.”

Kwa ushindi huo Simba SC inafikisha alama 38 ikiwa imecheza michezo 16 imeachwa kwa jumla ya alama sita na vinara Young Africans ambao wana alama 44 wakiwa wamecheza jumla ya michezo 18.

Mchezo wao unaofuata ni dhidi ya Azam FC utakaochezwa Jumapili Februari 07, Uwanja wa Mkapa na leo kikosi kitarejea Dar kutoka Dodoma kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wao ujao.

Biden atangaza muelekeo mpya siasa za Marekani
Uganda: Wanafunzi kuanza kurejea shuleni Machi