Wakati Mshambuliaji Kylian Mbappe akisumbua vichwa vya mabosi wa PSG hatma yake ikiwa haijulikani, taarifa zinadai mabosi wa klabu hiyo wapo kwenye mchakato wa kumsajili mshambuliaji wa Benfica, Goncalo Ramos mwenye umri wa maika 22, katika dirisha hili ili akaongeze nguvu eneo la ushambuliaji.

Ramos ambaye msimu uliopita alifunga mabao 27, alionyesha kiwango bora kwenye fainali za Kombe la Dunia zilizofanyika Qatar akiwa na timu yake ya taifa ya Ureno na kuwavutia vigogo vya barani Ulaya.

Hata hivyo, changamoĊ‚o kubwa inatajwa kufanikisha dili hilo ni kiasi cha fedha ambacho Benfica inakihuitaji, ambapo inadaiwa klabu hiyo inataka Pauni 80 milioni ili kumwachia Mshambuliaji huyo ambaye mkataba wake unamalizika mwaka 2025.

Kuna uwezekano mkubwa PSG ikamsajili Mshambuliaji huyo hata kabla ya kumpiga bei Mbappe kwani hata kama staa atabaki ndani ya viunga yya Princes Park huenda asitumike kwenye kikosi.

Mbappe alibaki Paris wakati timu yake iliposafiri kwenda barani Asia kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya, wakati hayo yakiendelea PSG ikatangaza kumuuza staa huyo wa kimataifa wa Ufaransa.

Katika dirisha lililopita la majira ya baridi vigogo mbalimbali pamoja na Manchester United vilionyesha nia ya kutaka kumsajili Goncalo Ramos.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Agosti 7, 2023
Maddison: Ningependa Harry Kane abaki