Google haitaruhusu tena vyombo vya habari vya serikali ya Urusi kuonyesha matangazo, kufuatia uamuzi kama huo uliofanywa Jumamosi na kampuni mwenza ya video ya YouTube.
“Ili kukabiliana na vita nchini Ukraine tunasitisha upatikanaji wa mapato wa Google kwa vyombo vya habari vinavyofadhiliwa na serikali ya Urusi kwenye mifumo yetu yote.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Google imesema kuwa ”Tunafuatilia kwa makini matukio mapya na tutachukua hatua zaidi ikihitajika.”
Tangazo hilo linakuja baada ya tangazo la hivi karibuni kwa vyombo vya habari vinavyohusishwa na Urusi huku kukiwa na wimbi la ukosoaji ulioelekezwa kwa majukwaa ya Big Tech katika wiki iliyopita kwa kuruhusu upataji wa mapato kuendelea licha ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.
Siku ya Ijumaa mtandao wa Meta (Facebook) ulisema utasitisha uwezo wa vyombo vya habari vya serikali ya Urusi kuendesha matangazo na kujipatia mapato kwenye majukwaa yake.