Muingereza Gordon Reid ameshinda mchezo wake wa pili katika mashindano ya walemavu ya Tennis Masters na kujiweka katika nafasi nzuri ya kuingia kwenye hatua ya nusu fainali itakayopigwa mjini Loughborough.

Baada ya kupoteza mbele ya Bingwa Joachim Gerard siku ya Jumatano, Reid amemshinda Nicolas Peifer wa Ufaranda kwa seti 3-6 6-4 6-3.

Muingereza mwenzake Andy Lapthorne naye pia amefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali baada ya kumchapa Heath Davidson wa Australia kwa seti 6-2 7-5.

Alfie Hewett na Lucy Shuker walipoteza michezo yao.

Hewett, namba mbili kwa ubora duniani kwa upande wa wanaume, alipangwa kucheza na Shingo Kunieda wa Japan lakini alipoteza kwa seti 2-6 6-4 6-2 baada ya kuumia bega.

Mwekezaji wa Simba kujulikana jumapili
Afisa Ugavi wa GGM ashikiliwa na Jeshi la Polisi