Jeshi la Polisi Nchini Afrika Kusini limeweka ulinzi mkali dhidi ya mke wa Rais wa Zimbabwe, Grace Mugabe anayekabiliwa na kesi ya kumshambulia mwanadada mmoja ambaye ni mwanamitindo nchini humo.
Ulinzi umeimarishwa katika mipaka yote ya nchi hiyo huku mazungumzo ya kidiplomasia yakiendelea baina ya nchi hizo kuhusu jinsi watakavyoweza kutatua tatizo hilo lililojikeza.
Aidha, polisi walitarajia kuwa mke wa Rais huyo angeweza kujisalimisha mwenyewe mikononi mwa jeshi hilo lakini mpaka sasa hajulikani alipo nchini humo hali iliyopelekea jeshi hilo kuimarisha ulinzi mipakani na viwanja vya ndege ili asiweze kutoroka.
Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe pia amewasili nchini humo kwaajili ya mkutano mkuu wa viongozi wa mataifa ya kusini mwa Afrika SADC unaotarajiwa kuanza mapema hii leo kujadili mambo mbalimbali.
-
Mke wa Mugabe awaponyoka polisi Afrika Kusini na tuhuma za kumpiga mrembo
- Odinga kutinga mahakamani kupinga matokeo
-
Serikali ya Zimbabwe yamkingia kifua mke wa Mugabe
Hata hivyo, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Afrika Kusini, Fikile Mbalula amesema kuwa polisi wameimarisha ulinzi katika mipaka yote na viwanja vya ndege ili kuhakikisha mke wa Rais huyo wa Zimbabwe hatoroki nchini humo.