Muamuzi mstaafu Graham Poll, amekitaka chama cha soka nchini England kufuatilia kwa ukaribu tukio la mshambuliaji wa klabu ya Chelsea, Diego Costa alilolifanya wakati wa mchezo wa ligi ya nchini humo dhidi ya Arsenal uliochezwa mwishoni mwa juma lililopita.

Poll, ametoa msukumo kwa FA kufanya hivyo kutokana na kukiri kuchukizwa na tabia ya utovu wa nidhamu wa mshambuliaji huyo ambaye alionekana kumuhadaa muamuzi Mike Dean na kufanikiwa kwa kuficha makosa yake.

Poll amesema Costa hakupaswa kuendelea kucheza katika mchezo huo kwani hata yeye alistahili adhabu ya kuonyeshwa kadi nyekundu, baada ya kumsababishia adhabu kama hiyo beki wa Arsenal Gabriel Paulista.

Amesema kabla ya tukio la kadi nyekundu kutoka kwa Paulista, mashambulaiji huyo kutoka nchini Hispania ambaye ni mzaliwa wa nchini Brazil alimpiga kibao cha uso Laurent Koscielny na kisha alimsukuma kwa makusudi.

Hata hivyo mstaafu huyo, amewashauri maafisa wa FA, kumfungulia mashtaka Costa ili kuuonyesha ulimwengu hakua na haki ya kuendelea kubaki mchezoni.

Emmanuel Mbasha Ashinda Kesi Ya Ubakaji
Martial Ampa kiburi Louis Van Gaal