Baada ya Diamond Platmumz kufanyiwa mahojiano maalumu na waandaaji wa Tuzo kubwa duniani za Muziki GRAMMYs , kupitia Website yao pamoja na kurasa zao za mitandao ya kijamii, Grammy wamemuelezea Diamond Platnumz kama mwanamuziki aliyeweza kubadilisha taswira ya Muziki wa Afrika Mashariki Pamoja na kufikia viwango ambavyo ni ndoto ya kila mwanamuziki kufika .

Grammys Pia wamesifu jitahada za Diamond, kuweza kuongezea ladha za Kiingereza na Kiswahili katika Muziki wa BongoFleva kitu kilichofanya aweze kuvuka mipaka na kufanya kazi na wasanii wakubwa duniani kama vile Omarion, Rick Ross, Ne-Yo na Alicia Keys.

Tuzo za Grammys ndio Tuzo kubwa zaidi za Muziki Duniani na ndoto ya kila mwanamuziki ! Hivyo kitendo cha waandaaji wa Tuzo hizi kumzunguzia na kumpa heshima Diamond Platnumz , ni ishara nzuri kwa Muziki wa Afrika Mashariki.

Rais Magufuli ampa pole Zitto Kabwe
Sven afunguka udhaifu wa wachezaji Simba SC

Comments

comments