Kiungo wa klabu ya Arsenal Granit Xhaka amehojiwa na jeshi la polisi jijini London, baada ya kutuhumiwa kwa kutoa maneno ya kibaguzi dhidi ya mfanyakazi wa uwanja wa ndege wa Heathrow.
Kiungo huyo kutoka nchini Uswiz, anadaiwa kufanya kosa hiyo usiku wa jumatatu, alipokua katika haratakati za safari yake ya kwenda nchini Ujerumani.
Xhaka alifika uwanjani hapo akiwa amechelewa na alikuta tayari utaratibu wa kufanyiwa huduma ya safari yake umeshafungwa, jambo ambalo lilimlazimu mfanyakazi anaedaiwa kutolewa maneno ya kibaguzi kumzuia na ndipo kadhia za ubaguzi zilipojitokeza.
Hata hivyo kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24, amekana kufanya kosa hilo.
Tukio hilo limetokea ikiwa ni baada ya siku moja, ambapo Xhaka aliadhibiwa kwa kuonyeshwa kadi nyekundu alipokua kwenye mchezo wa ligi kuu ya soka nchini England, kwa kumchezea ndovyo sivyo mchezaji wa Burnley.
Kadi hiyo imekua ya pili kwa mchezaji huyo kwa msimu huu wa 2016/17, lakini ni kadi yake ya tisa ndani ya miaka mitatu.