Wachezaji Granit Xhana na Xherdan Shaqir watacheza mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi dhidi ya Costa Rica, baada ya kamati ya nidhamu ya shirikisho la soka Duniani (FIFA) kushindwa kutoa hukumu dhidi yao.
Wawili hao waliingia katika mashaka ya kufungiwa michezo miwili, kufuatia aina ya ushangiliaji wao waliouonesha kwa ishara ya kukunja mikono ‘Eagle Style’ dhidi ya Serbia.
Ushangiliaji huo uliweza kuzua mjadala FIFA ukielezwa kuhusishwa na masuala ya kisiasa, ambayo yamekuwa yakipigwa vita katika mchezo wa soka na baadaye kutoka ripoti zilizoeleza kuwa FIFA imewafungia wachezaji hao.
Lakini kamati hiyo baada ya kukaa chini na kujadiliana kuhusiana na hukumu yao imebainika hawana makosa yoyote, na sasa wapo huru kuendelea na ratiba ya michuano hiyo.
Kikosi cha Uswiz kitashuka dimbani kesho jumatano kucheza mchezo wa mwisho wa kundi E dhidi ya Costa Rica, huku mchezo mwingine wa kundi hilo utakua Brazil na Serbia.