Kiungo Mshambuliaji wa Mchezaji wa Manchester United Mason Greenwood amekamatwa kwa tuhuma za ubakaji na shambulio kufuatia madai kwenye mitandao ya kijamii.

Polisi wa Greater Manchester walisema ilifahamishwa kuhusu “picha na video za mitandao ya kijamii zilizotumwa na mwanamke akiripoti matukio ya unyansaji wa kingono.”

Iliongeza “tunaweza kuthibitisha kuwa mwanamume mwenye umri wa miaka 20 amekamatwa kwa tuhuma za ubakaji na shambulio.”

Anaendelea kuzuiliwa kwa mahojiano na uchunguzi unaendelea. Manchester United hapo awali ilisema mchezaji huyo hatarejea kwenye mazoezi au mechi hadi ilani nyingine.

Klabu hiyo ilisema “haikubaliani na vurugu za aina yoyote” na imefahamishwa kuhusu madai hayo kwenye mitandao ya kijamii lakini haitatoa maoni yoyote zaidi hadi “ukweli utakapothibitishwa.”

Greenwood hajajibu madai hayo ya mitandao ya kijamii. Greenwood mwenye umri wa miaka 20, ambaye aliichezea klabu hiyo kwa mara ya kwanza Machi 2019, alisaini mkataba wa miaka minne Februari 2021 baada ya kupanda katika safu ya akademi ya United.

Mugalu: Ninapambana kurudi kwenye kiwango changu
ASFC: Simba, Young Africans zabaki Dar es salaam