Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Ufaransa na Klabu ya Atletico Madrid Antoine Griezmann, ameweka wazi kwamba hivi sasa yuko vizuri na anafurahia maisha kikosini hapo.

Griezmann alitupia mabao mawili wakati Atletico Madrid ikishinda kwa mabao 2-1 dhidi ya Almeria, katika Mshike Mshike wa Ligi Kuu nchini Hispania.

Kiungo huyo msimu huu ameonekana kurejesha makali yake akiwa kikosini hapo tangu amerejea kutoka FC Barcelona. Griezmann kwa sasa amefanikiwa kufunga mabao 10 ndani ya La Liga.

Huo ulikuwa ushindi wa sifa mfululizo kwa Atletico Madrid, huku ikiwa haijafungwa katika michezo 13 kwenye ligi hiyo. Griezmann amesema: “Nipo katika kiwango changu, kwa sasa ninafurahia kucheza hapa Atletico Madrid, nitatoa kila kitu ambacho kocha wangu ananielekeza ili kuwa bora zaidi.”

Mapigano yauwa 200, majengo ya Hospitali yaharibiwa
DC akerwa kushuka taaluma