Rais wa Makampuni ya GSM, Ghalib Said Mohammed usiku wa kuamkia leo Jumapili (Julai 11) aliwaandalia hafla maalum Wachezaji wa Young Africans, ili kuwapongeza.

GSM alifanya hivyo ikiwa ni muendelezo wa furaha ya kuifunga Simba SC kwenye mchezo wa Ligi Kuu uliounguruma Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, Jumamosi (Julai 03).

Young Africans iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya watani wa Jadi Simba SC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, bao likifungwa na Kiungo Zawadi Mauya dakika ya 11.

Pia hafla hiyo iliyofanyika kambini Avic Town, Kigamboni jijini Dar es salaam, imetumika kama kuwatakia kheri wachezaji wa Young Africans kwenye michezo miwili iliosalia dhidi ya Ihefu FC na Dodoma Jiji FC kabla ya kumaliza msimu huu 2020-21.

Mbali na michezo hiyo ya Ligi Kuu Tanzania Bara, Young Africans itacheza mchezo wa Fainali Kombe la Shirikisho (ASFC) dhidi ya Simba SC mkoani Kigoma Julai 25.

Wakandarasi wahimizwa kumaliza miradi kwa wakati
Wanafunzi 102 wanusurika kifo Morogoro