Mwenyekiti wa makampuni ya GSM, Galib Said Mohammed ‘GSM’ amesema uwekezaji wake ndani ya klabu ya Young Africans lengo kuu ni kuona timu hiyo inaondoka katika changamoto za kiuchumi na kuweza kujitegemea.

Ghalib amekuwa mtu muhimu sana kwa Young Africans tangu msimu uliopita, kampuni yake ikihusika katika usimamizi wa timu pamoja na kuchukua jukumu la kusimamia mchakato wa Mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji.

GSM pia imeingia makubaliano na Young Africans kusimamia mauzo ya jezi pamoja na bidhaa nyingine zenye nembo ya Young Africans.

Ghalib amebainisha kuwa hakuna faida kubwa anayoipata Young Africans lakini yote anayofanya ni kwa ajili ya mapenzi yake kwa klabu hiyo kongwe katika ukanda wa Afrika Mashariki na kati.

“Ukija na wazo la kupata faida kwenye timu zetu hizi unajidanganya, tunasaidia hizi timu kwa sababu tunazipenda. Ndio maana tumewaleta La Liga ili kujenga mfumo imara utakaokuwa na manufaa huko mbeleni,” alisema Ghalib katika mahojiano ya ana kwa ana na Mwanahabari Privaldinho

Aidha Ghalib amewaalika Wawekezaji wengine wenye nia ya kuisaidia Young Africsna wajitokeze ili waunganishe nguvu kutengeneza taasisi imara.

“Nimezisikia taarifa za Manji (Yusufu) kutaka kurudi Young Africans, binafsi nimefarijika sana, kama akirudi, ujio wake utakuwa msaada mkubwa kwa klabu. Sio Manji tu, yeyote mwenye nia ya dhati ya kuisaidia, aje tuungane kwa pamoja kwani mshikamano huleta maendeleo maradufu.”

Fraga atuma ujumbe Simba SC
Madereva bajaji, bodaboda walalamikia tabia za askari barabarani