Kampuni ya GSM imeuandika barua rasmi uongozi wa klabu ya Young Africans na kueleza kuanzia sasa itafanya yale ambayo yapo kwenye mkataba na klabu hiyo.
Miongoni mwa mamboa mbayo yametajwa kuwa nje ya mkataba na yalikua yakifanywa na kampuni hiyo ni Suala la usajili wa wachezaji, kambi ya timu, gharama za uwanja wa mazoezi, tiketi za ndege kwa benchi la ufundi na wachezaji.
Mpango wakuzingatgia yaliopo kwenye mkataba wa pande hizo mbili, umeanza kufanyiwa kazi rasmi jana Jumanne (24 March 2020), baada ya kuwasilishwa kwa barua.
Barua hiyo imefafanua changamoto zilizowahi kurekebishwa na kampuni ya GSM nje ya mkataba ni:
1. Kumrudisha LAMINE baada ya kutukatiza mkataba wake.
2. Kusajili wachezaji katika kuiongezea nguvu klabu yetu. I.Bernad Morisson. II.Ditram Nchimbi III.Haruna Niyonzima IV.Adeyum Saleh
3. Kuwaleta na kulipa gharama zote za KOCHA MKUU,KOCHA WA MAZOEZI NA VIUNGO (FITNESS COACH na PHYSIO)gharama hizo ni pamoja na mishahara, nusafiri wa ndani,nyumba na ticket za kwenda na kurudi makwao(BELGIUM & SOUTH AFRICA).
4. Kulipa Mishahara.
5. Kulipa Bonas za ushindi ktk mechi zote timu iliposhinda kuanzia Mwezi Desemba 2019.Pamoja na ahadi kubwa ya ushindi kwa mechi dhidi ya watani wa jadi na kuitekeleza baada ya ushindi huo.
6. Kulipa gharama zote za CAMP/HOTEL kwa timu kuanzia mwezi Desemba 2019.
7. Tiketi za ndege kwa wachezaji na viongozi.
8. Kulipa na kugharamia uwanja wa mazoezi kwa ukamilifu wake.Hii ni pamoja na ukarabati wa uwanja na ununuzi wa vifaa vya mazoezi.
9. Kulipa baadhi ya madeni ya nyuma ya usajili wa wachezaji. Aidha,yote hayo yamekua yakifanyika kwa MAPENZI MEMA kwa klabu yetu bila kujali gharama nyingi na kubwa tunazolipa.