Meneja wa Mabingwa wa Soka nchini England Manchester City Pep Guardiola anaamini Lionel Messi atarudi FC Barcelona akapewe ufalme wake anaostahili baada ya kutimkia Paris Sait-Germain ya Ufaransa.

Hatima ya Messi kwa sasa bado haijulikani ndani ya klabu hiyo baada ya kupewa adhabu kwa kusafiri kwenda Saudi Arabia bila ya ruhusa.

Taarifa ziliripoti Messi amekubali kuondoka PSG msimu utakapomalizika, lakini baba yake mzazi amekana madai hayo akidai ni uzushi, huku Guardiola akisisitiza Messi atafanya juu chini arejee Nou Camp.

Guardiola amesema kupitia kituo cha televisheni cha ESPN: “Nina tiketi zangu za mechi Nou Camp, naamini siku moja nitaagana naye kwa staili ya aina yake, ni mchezaji bora duniani wa muda wote.

Ndani ya miaka 12 iliyopita FC Barcelona ingekuwa sio kitu bila ya Messi, matumaini yangu siku itafika nitakuwa kwenye kiti uwanjani nikimpigia makofi Nou Camp, najua Joan Laporta atajaribu kumrudisha Messi, na familia yake itapokewa kwa mapenzi makubwa.”

Wakati huo huo, PSG ilikataa kuzungumzia kuhusu tetesi za Messi kuhusishwa na Al-Hilal ya Saudia na ikasisitiza kwamba bado nyota huyo ana mkataba utakaodumu hadi Juni 30.

14 Wafariki kwa ajali ya basi, idadi yahofiwa kuongezeka
Kikwete atembelea ubalozi wa Tanzania Korea Kusini