Kocha wa klabu ya Manchester City Pep Guardiola amesaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo mpaka mwaka 2021.
Guardiola alijiunga na Manchester City mwaka 2016 na hii inamaanisha baada yakuongeza mkataba itakuwa ni mara ya kwanza kwa kocha huyo kukaa katika klabu moja kwa muda mrefu akiwa kocha ambapo awali amezifundisha timu za Barcelona na Bayern Munich.
”Ninajiskia vizuri kuwa hapa, ninafurahi kufanya kazi na wachezaji kila siku na tutazidi kufanya vizuri miaka ijayo”, alisema Guardiola.
Muhispania huyo mwenye umri wa miaka 47 ameiwezesha Man City kuchukua ubingwa wa ligi kuu ya Uingereza katika msimu uliomalizika kwa rekodi yakipekee yakufikisha pointi 100.
City wameweka rekodi ya kufunga mabao 106 nakushinda michezo 32 wakiwa wamepoteza pointi 14 tu katika ligi kuu ya Uingereza jambo amablo linamfanya Pep kuwa kocha bora wa EPL.
Katika msimu wake wa kwanza akiwa kocha Pep aliiongoza City kumaliza msimu katika nafasi ya tatu katika msimamo wa ‘EPL’ jambo ambalo mwenyekiti wa Man City Khaldoon al-Mubarak.