Meneja wa klabu ya Manchester City Josep “Pep” Guardiola Sala anaongoza kwenye orodha ya mameneja wanaolipwa mshahara mkubwa kwa juma, katika Ligi Kuu ya England.

Guardiola ambaye aliajiriwa Etihad Stadium mwaka 2016 akitokea kwa mabingwa wa Ujerumani FC Bayern Munich, imebainika ndio meneja anaelipwa mshahara mkubwa, akichukua kiasi cha Pauni 417,500 kwa juma, sawa na Pauni 1,670,000 kwa mwezi.

Meneja wa mabingwa wa Ligi ya England kwa sasa (EPL) Jurgen Klopp, anafuatia kwenye orodha hiyo akilipwa mshahara wa Pauni 313,500 kwa juma, sawa na Pauni 1,254,000 kwa mwezi.

Orodha ya michahara ya baadhi ya mameneja wanaofundisha kwenye klabu za ligi ya England, walioingia kumi bora.

  1. Pep Guardiola – Pauni 417,500 (Kwa juma).
  2. Jurgen Klopp – Pauni 313,500 (Kwa juma).
  3. Jose Mourinho – Pauni 313,000 (Kwa juma).
  4. Carlo Ancelotti – Pauni 230,000 (Kwa juma).
  5. Frank Lampard – Pauni 166,850 (Kwa juma).
  6. Marcelo Bielsa – Pauni 166,660 (Kwa juma).
  7. OleGunnar Solskjaer – Pauni 160,000 (Kwa juma).
  8. Bendan Rodgers – Pauni 105,000 (Kwa juma).
  9. Mikel Arteta – Pauni 105,000 (Kwa juma).
  10. Roy Hodgson – Pauni 93,750 (Kwa juma).
TCRA, NEC wawafunda watoa huduma ya habari mitandaoni
TANZIA: Mgombea ubunge afariki dunia

Comments

comments