Washambuliaji Lonel Messi na Erling Haaland wote wanastahili kushinda tuzo ya Ballon d’Or, kwa mujibu wa Kocha Mkuu wa Manchester City, Pep Guardio Messi alikuwa nahodha wa Argentina na kutwaa ubingwa wa Kombe la Dunia nchini Qatar huku Haaland akifunga mabao 52 katika michezo 53 na kuisaidia City kushinda mataji matatu (Ligi Kuu England, Ligi ya Mabingwa Ulaya na Kombe la FA).
Messi na Haaland ndio watu wawili wanaopendekezwa zaidi katika tuzo hiyo ambayo itatangazwa katika hafla itakayofanyika Oktoba 30, mwaka huu na Guardiola anasema wachezaji wote wawili wa- nastahili kushinda.
“Siku zote nilisema Ballon dor inapaswa kuwa katika sehemu mbili; moja kwa Messi, kisha baada ya nyingine ili Haaland ashinde,” alisema Guardiola wakati akizungumza na waandishi wa habari.
“Tulishinda tatu, alifunga mabao milioni. Msimu mbaya zaidi kwa Messi ni bora zaidi kwa wachezaji wengine. Wote wanastahili. Kiuhalisia nataka Haaland awe nayo kwa sababu alitusaidia kufikia kile tulichopata, ningependa lakini Messi alishinda Kombe la Dunia.”
Haaland aliifungia Norway mabao mawili katika ushindi wa 4-0 dhidi ya Cyprus wakati wa mapumziko ya kimataifa na Guardiola atatumaini itarudisha tena kiwango akiwa na City baada ya kucheza mechi tatu bila bao, Brighton walikuwa wageni wa City kwenye uwanja wa Etihad juzi Jumamosi (Oktoba 21).